Kuhusu mgodi

Geita, mojawapo ya migodi ya kwanza ya AngloGold Ashanti, unapatikana kaskazini magharibi mwa Tanzania, katika viwanja vya dhahabu vya Ziwa Viktoria katika mkoa wa Geita. Mgodi huu umekuwa ukiendeleza shughuli kama mgodi mkubwa tangu miaka ya 1930.

Aunsi milioni 7.7 za dhahabu zimeshazalishwa tangu tuanzishe mgodi huu rasmi mwaka 2000. Kufikia Disemba 2016 Raslimali ya Madini ilikuwa ni wakia milioni 7.32.

Dhahabu iliyoko kwenye mgodi wa Geita ilichimbwa kutoka kwenye mashimo kadhaa yaliyo wazi tu hadi mnamo mwaka wa 2015. Tangu hapo hadi sasa, Geita imeweza kubadilisha uchimbaji na kuwa uwewa chini ya ardhi katika eneo la Star & Comet na mwaka wa 2017 utakuwa ndio mwaka mzima wa kwanza wa uzalishaji wa kibiashara kutoka chini ya ardhi.

Kazi ya maandalizi ya kufikia dhahabuya chini ya ardhi kwenye shimo la Nyankanga imekamilika na shughuli za kulipua zimeanza rasmi mwaka wa 2017.

Mgodi wa Dhahabu wa Geita unajizalishia kawi yake na mfumo wa kusimamia nishati upo ili kusaidia maendeleo ya siku za usoni.

Pakua: Maelezo mafupi kuhusu Profaili ya Kiundeshaji ya 2016: Geita
Aunsi zilizozalishwa kila mwaka
2000 2001 2002 2003 2004 2005 2006 2007 2008 2009 2010 2011 2012 2013 2014 2015 2016 177 546 579 661 692 613 308 327 264 272 357 494 531 459 477 527 489 Uwekezaji kwa ajili yauendelezaji Ahueni Poromoko kubwa la ukutawa chimbo likifuatwa namarekebisho Kuanzisha na kuzidisha

Historia ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita

Michango yetu nchini Tanzania

Pesa Taslimu zilozowekezwa na kusambazwa kuanzia 2000
2016 2014 2012 2010 2008 2006 2004 2002 2000 1200 1000 800 600 400 200 0 (200) (400) 45% 55% Mgao wa Serkali ya Tanzania Mgao wa AngloGold Ashanti Haujumuishi gharama ya kupata
Tazama mchakato wa malipo ya mkuo wa dhahabu na mrabaha

Mchakato wa malipo ya mkuo wa dhahabu na mrabaha

Uthibitishwa na serikali katika kila Hatua

 • 1

  Mikuo ya dhahubu inapakiwa

  • Uthibitishaji wa uzito wa mikuo ya dhahabu
  • Visanduku vinafungwa na uzito kurekodiwa

  verifiedna MEM, TMAA, TRA na Mgodi wa Dhahabu wa Geita

 • 2

  Ankara, orodha ya vilivyopakiwa na hati za muda za mrabaha zinatayarishwa

  approvedna maafisa wa serikali na Mgodi wa Dhahabu wa Geita

 • 3

  Mirabaha ya muda

  Paidkwa serikali ya Tanzania

 • 4

  Hati na risiti za bidhaa nje zinatengenezwa

  approvedZinathibitishwa tena na ankara iliyotolewa na TRA na hati ya kuachilia bidhaa kutengenezwa

 • 5

  Iliyosafirishwa

  Dhahabu iliyosafirishwa Kutoka Julius Nyerere International hadi Afrika Kusini

 • 6

  Iliyosafishwa

  Dhahabu huoshwa nchini Afrika Kusini na Kiwanda cha Kusafisha cha Rand

 • 7

  Dhahabu iliyouzwa

  Habari kuhusu viwango, bei, na dhamani iliyorekodiwa

  approvedData iliyopeanwa kwa Serikali ya Tanzania

 • 8

  Mapato yanarekodiwa

  Mirabaha inalipwa kulingana na mauzi halisi

  Paidkwa serikali ya Tanzania

Mlipaji kodi Mkubwa

Kila mara, AngloGold Ashanti imekuwa ni mojawapo ya Kampuni Kinara katika ulipaji kodi Mkubwa sawa na sheria na taratibunchi ya Tanzania.

Jinsi ambavyo tumeshiriki mapato ya mauzo ya dhahabu Dola bilioni $6.967 - Jumla ya mapato ya muazo ya dhahabu
Maendeleo ya mgodi na vifaa 20.1% Riba ya mkopo na ada 1.9% Mafuta 12.5% Dola bilioni 1.1 imelipwa kwa Serikali ya Tanzania 15.3% Migawio iliyolipwa kwa Anglogold Ashanti 12.5% Nyenzo 15.8% Kazi 4.8% Wakandarasi 14.9% 37.7% Value shared with other Tanzanian stakeholders Huduma 2.2%
 • Dola bilioni 1.1 Jumla ya malipo kwa serikali

 • dola milioni 225 Mirabaha iliyolipwa
 • dola milioni 136 Kodi za mapato ya ajira
 • dola milioni 367 Kodi ya makampuni iliyolipwa
 • dola milioni 8 Malipo ya leseni ya uchimbaji
 • dola milioni 121 kodi ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ya nchi iliyolipwa
 • dola milioni 6 Ada ya Baraza la Wilaya ya Geita

Mwajiri anaewajibika

Kazi 9,000
za moja kwa moja au zingine zilizoundwa

Wafanyakazi 3,748
1,748 wa kudumu (wa muda mrefu)
2,100 wa muda mfupi
 • Nafasi ya pili Katika Tuzo ya ATE ya 2016 ya Mwajiri Bora wa Mwaka
 • Mwajiri Mlipaji Makini na kwa wakati katika sekta ya uchimbaji na Mfuko wa Kitaifa ya Usalama wa Kijamii
 • Huwa tunajitahidi kudumisha usalama na afya ya waajiriwa wetu
 • Asilimia 96 ya wafanyakazi wetu ni Watanzania
 • Asilimia 55 ya timu ya wasimamizi wakuu ni Watanzania
 • KAMATI KUU YA MGODI WA DHAHABU WA GEITA

KAMATI KUU YA MGODI WA DHAHABU WA GEITA

R Jordinson (UK)

Mkurugenzi Mtendaji

H Cawood (SA)

Meneja wa Uendeshaji

S.Shayo (TZ)

Meneja Mkuu Uendelevu

N.J. Shilla (TZ)

Meneja HME

E. Ankamah (GH)

Meneja wa Fedha

G. Lyimo

Msimamizi wa Kodi

D. Nzaligo (TZ)

Mshauri Mkuu wa Kisheria

C. Masubi (TZ)

Meneja HR (Raslimali W)atu

C. Duvel

Manager Geology

Dr. K. Mvungi (TZ)

Msimamizi wa HSET

C. Steyn (SA)

Usalama wa Msimamizi

M. Ndoroma (TZ)

Msimamizi wa SEPT

Inaendesha biashara ya ndani

AngloGold Ashanti inasaidia na kuwezesha biashara za ndani Mtandao wa wauzaji wa ndani uliongezeka hadi wamiliki biashara 305 Watanzania

Programu ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Geita

Dola milioni 183 zilitumiwa na wauzaji wa ndani mwaka wa 2016

Huduma za ndani:

 • Ujenzi
 • Visehemu na huduma
 • Chakula na upishi
 • Uchukuzi
 • Malazi
 • Matibabu
 • Huduma za Teknolojia ya Habari na Huduma za Raslimali Watu

Mradi wa maji safi kwa matumizi ya ndani

Mradi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita wa maji safi unalenga kuwasambazia maji wakazi wa mji wa Geita kwa njia ya miunganisho ya kinyumbani na vibanda vya umma. Jamii za watu kutoka sehemu mbalimbali wanaishi Mjini Geita nchini Tanzania. Mji huu unavutia wachimbaji wadogo, wafanyabiashara, na wakulima na kwa sasa zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita wanaishi mjini Geita Hata hivyo, mji huu bado haujajitosheleza kuwapa wakaazi wake huduma za kijamii. Wakati mradi wa maji safi ulipoanza mwaka 2012, asilimia3 tu ya wakaazi ndio walioweza kupata maji safi na salama ya mfereji. Kwa sasa, baada ya mtandao wa usambazaji kukamilika, na mradi kuzinduliwa Januari 2016, asilimia ya waliofikiwa na huduma imefika 36. Asilimia hii inakomea hapo kwa sababu ya ongezeko la idadi ya watu mjini kutoka 80,000 hadi 192,000 tangu mradi uanzishwe hadi sasa. GGM imeshatumia dola milioni 5.2 (Shilingi Bilioni 12) kufadhili mradi huu hadi hatua iliyoko sasa.

Wazo la mradi huu lilitokana na mijadala ya Kamati ya Mahusiano ya Jamii (CRC). CRC inajumuisha wataalam wa serikali wanaofanya kazi katika Wilaya ya Geita na wanatimu wa timu ya uendelevu wa GGM. Baraza hili linasimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita. Kwa sababu ya umuhimu wake wakati huo, ukosefu wa maji ulichukuliwa kuwa changamoto kubwa iliyowakumba wanajamii wa Geita. Kwa hivyo, uamuzi ulifanyika kwamba serikali na GGM ifadhili mradi huo kwa pamoja, na mkataba wa makubaliano ukatiwa saini kulingana na hayo. Jukumu la GGM mwanzoni lilikuwa kujenga kisima cha kuhifadhia, pamoja na kujenga mitambo ya kusafisha na kuchuja maji na kuimarisha bwawa la Nyankanga.

Bada ya mradi kukamilika, , sehemu kubwa ya Tanzania ilikumbwa na ukame mnamo mwaka wa 2016 na mojawapo ya maeneo yaliyoathirika mno lilikuwa eneo la Ziwa Victoria, linalojumuisha Geita hivyo ukame ukaathiribwawa la Nyankanga, ambalo ni hifadhi na chanzo cha maji kwa mradi wa Mji wa Geita. Hivyo basi ilikadiriwa kwamba ifikapo Agosti 2017 viwango vya bwawa vitakuwa chini mno na hata kushindwa kutoa maji yoyote kwa ajili ya mradi, basi mpango mpya wa kugawa maji Mjini Geita kuanzia Juni 2017 ulianzishwa kama mbinu ya kuhifadhi maji. Ili jamii ziwe na maji ya kutosha, Mgodi wa Dhahabu wa Geita uliamua kufunga bomba la pili la kilomita 24 kutoka Ziwa Viktoria hadi kwenye mitambo ya ya kusafisha maji kwa gharama ya dola za Marekani milioni 3.5. (Shilingi Bilioni 8) Bomba hilo litakuwa na ujazo wa mita 250 ya mchemraba kwa saa na litahakikisha usambazaji wa maji ya kutosha kwa Mji wa Geita, bila kujali changamoto za hali ya hewa. Mradi umeanzakutarajiwa kukamilika mwanzo mwa robo ya nneu ya 2017.

Shule ya Wasichana ya Nyankumbu

Majadiliano yaliyosababisha ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Nyankumbu yalianza katika baraza la Kamati ya Uwekezaji katika Jamii (CRC) vikao vilivyopita Wakati huo, kama ilivyo sasa, wasichana katika eneo la Geita walikuwa na nafasi chache za kupata elimu kuliko wavulana, kwa sababu ya baadhi ya tamaduni za kijamii. Wakati wavulana wakipewa muda wa kucheza au kushiriki katika masomo na matayarisho nyumbani baada ya saa za shule, wenzao wa kike walitarajiwa kusaidia familia katika kazi za nyumbani. Utaratibu huu wa kijamii katika kiwango cha familia ulisababisha kufeli kwingi kwa wasichana katika mitihani yao ya shule. Hali hiyo ilizoroteshwa zaidi na wazazi walioona kwamba kupeleka wasichana shuleni ni kupoteza muda kwa sababu ufaulu wao ulikuwa ni mdogo.

Mambo haya yalisababisha kamati ya CRC kuamua kuanzisha shule ya wasichana inayolenga kufunza sayansi. Shule hii ilikuwa iwe na bweni ili kuhakikisha kwamba wasichana wanaweza kutumia muda wao mwingi kusoma. GGM ilijitolea kufadhili ujenzi, huku serikali ikikubali kutoa ardhi na kuendesha shule kulingana na mtaala wa shule za umma. Wafanyakazi na mahitaji mengine yanatolewa na serikali. Kwa sasa, shule hii inasajiliwanafunzi kutoka wilaya zote tano ndani ya Eneo la Geita kwa ajili ya elimu ya sekondari ya kawaida kulingana na utendaji. Shule hii pia inatoa elimu ya kiwango cha juu kwa wasichana kutoka kote nchini. Hadi shughuli zake za mwanzo, muundo msingi wa shule uligharimu takriban dola milioni 5.5 za Marekani milioni (Shilingi Bilioni 12) na GGM inaendelea kusaidia shule katika jitahada zake za kuboresha utendaji. Msaada kama huo ni pamoja na urekebishaji wa maktaba, utoaji wa kompyuta, kuboresha uwezo wa waalimu, Mafuta ya dizeli ya kuendesha jenereta ya shule, na maji wakati wa mgawo.

Katika Mwaka wa 2017, shule ilikuwa na jumla ya wanafunzi 820 wa bweni na 47 wa kutwa. Wastani ya wanafunzi 160 wamehitimu kila mwaka tangu shule ianzishwe mwaka wa 2014. Shule bado haijatoa matokeo mazuri kama ilivyotarajiwa na waanzilishi wa wazo hilo. Vipengele kadhaa bado vinazuia utendaji wa kimasomo, kama vile uhaba wa waalimu bora, masuala ya sera, wafanyakazi wachache, na ubora wa wanafunzi walioandikishwa. Wadau wa maendeleo, ikiwa ni pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Geita, wanaendelea kushiriki na kutafuta njia za kuboresha utendaji wa kimasomo wa shule ili kupata faida kwa fedha zilizotumiwa katika mradi huu mkubwa. Mnamo Julai, 2017 ofisi ya Kamishna wa Eneo la Geita ilianzisha utafiti unaofanywa na Open University of Tanzania (Chuo Kikuu Huria cha Tanzania) uliofadhiliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita ili kugundua njia bora zaidi ya kuboresha utendaji wa shule na kushughulikia maswala mengine ya uendelevu wa shule.

Uimarishaji wa Hospitali ya Eneo la Geita

Mgodi wa Dhahabu wa Geita ulifanya matengenezo makubwa ili kufanya Hospitali ya Eneo la Geita kuwa ya kisasa iliyojengwa mwaka wa 1957. Mgodi ulifadhili vifaa vya matibabu vya kisasa vitakavyotumiwa katika uchunguzi na matibabu ya moyo, Utaalam wa meno na magonjwa mengine vifaa ambavyo vitakavyohakikisha kwamba wanajamii watapokea huduma maalum za afya ambazo hapo awali zilipatikana tu katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili (MOI) jijini Dar Es Salaam. GGM imewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 1 ya Tanzania katika mradi huu. Jamii ya Geita ina wakazi zaidi ya milioni 1.7 watakaonufaika na huduma za Hospitali ya Geita.

Upandaji Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kupambana na VVU/UKIMWI

Kilimanjaro Challenge inayosimamiwa kwa ushirikiano kati ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na wadau wengine, ni tukio la kila mwaka tangu 2002, tukio lililo kubwa zaidi katika sekta binafsi la kutoa msaada kwa ajili ya walioathirika na VVU katika Afrika Mashariki. Upandaji wa Mlima Kilimanjaro ni safari ya siku sita kwa wapandaji wakijumuisha waajiriwa wa Mgodi wa Geita wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa ujasiri ili kuchanga pesa za kusaidia serikali katika kupambana na VVU/UKIMWI. Kwa misaada ya mamia ya wadhamini, Mashirika zaidi ya 30 yasiyo ya kiserikali yamefaidika kutokana na mpango huo. Mnamo Mwaka wa 2016, takriban TZS milioni 750 zilisambazwa kwa wafadhiliwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kituo cha watoto yatima cha Moyo wa Huruma, Baraza la Wilaya ya Geita, TACAIDS, Taasisi ya Benjamin Mkapa na Hospitali ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Kibong’oto inayotumika kama Kituo cha Kitaifa cha Utafiti na Matibabu ya Kifua Kikuu TB na VVU/UKIMWI ni magonjwa yanayohusiana kwa ukaribu.

Siku za usoni

“Kwa miongo miwili iliyopita, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) umekuwa uwekezaji muhimu sana kwa AngloGold Ashanti. Mbali na kuwa mojawapo ya migodi yetu ya kwanza, Mgodi huu pia ni mfano mwema wa uwekezaji mzuri katika sekta ya uchimbaji. Kutokana na jitihada za watu wetu, wanaojikakamua kuwatumikia na kuwasaidia wanajamii wa Geita kila siku, na uwekezaji unaoendelea, tumeweza kuifanya GGM kuwa mgodi wa dhahabu wenye sifa barani Afrika.” Srinivasan Venkatakrishnan, CEO

Soma barua kutoka kwa CEO wetu
 • Wajibu wa kudumu kwa maendeleo ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita na kwa Tanzania
 • Uwekezaji wa dola milioni 43 katika kiwanda cha kuzalisha kawi
 • Kazi zaidi ya uchunguzi na miundo ya chini ya ardhi katika mawe yenye madini ya Nyankanya na Geita Hill
 • Maendeleo ya chini ya ardhi yanaendelea ili kuongeza maisha ya mgodi

Barua kutoka kwa CEO wetu

Kwa miongo miwili iliyopita, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) umekuwa uwekezaji muhimu sana kwa AngloGold Ashanti. Mbali na kuwa mojawapo ya migodi yetu ya kwanza, Mgodi huu pia ni mfano mwema wa uwekezaji mzuri katika sekta ya uchimbaji. Kutokana na jitihada za watu wetu, wanaojikakamua kuwatumikia na kuwasaidia wanajamii wa Geita kila siku, na uwekezaji unaoendelea, tumeweza kuifanya GGM kuwa mgodi wa dhahabu wenye sifa barani Afrika.

Lengo letu katika Geita ni kukuza sekta ya uchimbaji wa dhahabu nchini Tanzania ili ifanikiwe na kuwa imara zaidi. Tunaamini kwamba jukumu letu kama wanabiashara, na mojawapo wa wawekezaji muhimu sana nchini Tanzania, ni kuwezesha na kusaidia malengo ya nchi ya kuwa na uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka wa 2025. Kwa bidii na kujitolea, pamoja na ushirikiano na serikali, GGML inaweza na itachangia maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na kuboresha hali ya wananchi wake. Mbali na kunufaisha kampuni na wadau wake, faida zetu pia zinanuiwa kuwanufaisha wanajamii waliopo. Mafanikio ya GGM huhusishwa na ufanisi wa wanajamii na uhusiano na serikali.

Tunaamini kwamba Geita Gold Mining Limited (GGML) na AngloGold Ashanti zimetoa mfano mzuri na njia thabiti zinazoonyesha jinsi ambavyo sekta ya uchimbaji inaweza kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yaliipa GGM tuzo ya mlipaji kodi mwaminifu na mtiifu nchini. Isitoshe, GGM ilipewa tuzo ya Mwajiri Bora Namba 2 wa Mwaka wa 2016 na Chama cha Waajiri Tanzania, na ilipewa tuzo ya mwajiri mtiifu zaidi katika sekta ya uchimbaji na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. Haya yote hayangewezekana bila kuwepo kwa Timu ya wasimamizi wakuu ambayo asilimia 60 ya wanakamati wakuu wake ni Watanzania. Kutokana na uongozi wake, GGM imetambulika kama kampuni inayozingatia usalama na afya, na Occupational, Health and Safety (OHS) kwa miaka miwili mfulululizo, kutambulika kwa hivi majuzi kabisa kukiwa kwa 2017.

GGM inayonawiri, inayopokea faida zinazohitajika za uwekezaji, inayozalisha bidhaa kwa viwango fanisi zaidi viwezekanavyo na kulipa kodi kwa mtoza kodi, ndiyo mojawapo ya mbinu shupavu zaidi ya kuisaidia nchi kutimiza malengo yake. Huku tukijitosa katika mkakati huu mgumu na kuwekeza mamia ya mamilioni ya dola kadhaa katika GGM ili kuendeleza maisha ya mgodi huu wa dhahabu wa kipekee wa Tanzania, tunaelewa kwamba katika ulimwengu wa sasa sio rahisi kuendesha kampuni ya uchimbaji. Ili ufanikiwe na ulete mabadiliko ya kudumu kwa wanajamii na nchi unapoendeshea shughuli, lazima utekeleze shughuli zingine za maendeleo. Hili ni jambo ambalo washiriki wenzangu wa kazi katika AngloGold Ashanti wanalitetea kwa vyovyote vile. Ndio maana GGML imewekeza pakubwa katika sekta kuu zifuatazo mjini Geita: elimu, afya na muundo msingi. Tutashughulikia sana sekta hizi tatu katika siku zijazo kwa ajili ya watu wa Geita na Tanzania, sekta hizi pia ndizo zilizoko katika mipango muhimu ya serikali ya maendeleo.

Kwa miaka mingi, GGML imekuwa ikibadilisha maisha ya watu nchini Tanzania, pale ambapo mipango ya kielimu ya GGML imekuwa ikiimarisha jamii mbalimbali mjini Geita kwa kuwapa ujuzi na stadi za kuwasaidia kutimiza maono yao wenyewe na kusimamia maisha yao ya baadaye. Juhudi muhimu zaidi ya GGML hadi leo hii, itakayoleta mabadiliko makubwa na ya kudumu kwa siku zijazo, ni ujenzi wa GGML wa Shule ya Sekondari ya Nyankumubu ya wasichana uliogharimu dola Milioni 7. Shule hii ya kipekee, kwa maoni yangu, inapaswa kuwa mfano mzuri kwa shule za baadaye za sekondari kote nchini kimuundo msingi, kiujenzi na kwa vifaa. Wasichana wadogo walioko katika Eneo la Ziwa tayari wanavutiwa na shule hii. Ninamkumbuka binti mmoja mwerevu, anayeitwa Janeth G. Joseph, aliyejiunga na Chuo Kikuu cha Jordan huko Morogoro baada ya kukamilisha masomo yake kwa mafanikio shuleni Nyankumubu. Janeth bado huwa anatembelea Shule ya Sekondari ya Nyankumubu; pia huwa anafundisha hapo, hili alilolianzisha ninaamini kwamba litaendelea katika siku zijazo. Bila shaka, kazi hii si rahisi na kuna mengi bado ya kufanywa shuleni Nyankumubu - vifaa bora huwa havichangii elimu bora vyenyewe tu. Kwa sababu hiyo, lengo la GGML katika miaka michache ijayo, huku ikishirikiana kwa karibu na mamlaka ya ndani, litakuwa kuimarisha ubora wa elimu ili wasichana wote wanaohudhuria shule yetu wawe na uhakika kwamba watahitimu katika elimu ya juu.

Mojawapo ya mipango iliyobuniwa kwa ushirikiano na serikali ya ndani na wanajamii wenyeji ni mpango wa miaka mitano wa kuanzisha ushonaji, uunganishaji wa chuma kwa kufua, utengenezaji na biashara ya uundaji wa matofali kupitia Kituo cha SME cha Magogo. Kituo hiki, kilichoanzishwa mwaka wa 2016, kitawafunza na kuwasaidia wajasiriamali wadogo mjini Geita na kuwapa vifaa ili waboreshe stadi zao na kuwatayarisha waanze biashara zao wenyewe. Tukisalia katika ujasiriamali, GGML pia imeunda nafasi ndani ya kituo hiki itakayowapa kundi la wanawake fursa ya kuanza biashara ya upishi. Mwanzoni, kituo hiki ndicho kitakachonufaika na huduma hii, kisha hapo baadaye, huduma hii itawafikia wanajamii wengine. Huu ni mfano mwingine tu wa kile kinachosaidia lengo letu kuu la kuimarisha uwezo na kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi ya siku za usoni za Geita kando na uchimbaji.

Pia ni jambo la kufurahisha sana kuwaona wakulima wa karibu wakitumia stadi zilizoletwa kupitia Mpango wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Geita (Geita Economic Development Plan). Ukulima ni jambo muhimu sana nchini Tanzania na tunatambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kutokana na mbinu mpya zilizotumiwa kuimarisha ubora na wingi wa mazao yao – na hata kuanza kupanda mazao mapya ya kibiashara kama vile alizeti – wameimarisha taaluma za mababu zao kabisa na wameanza kuunda mfumo endelevu wa biashara ya kilimo.

Kusaidia wanajamii hawa ili waweze kukidhi mahitaji yao muhimu bila shaka ni jambo linalopaswa kufanywa, lakini kuwasaidia kupata ujuzi na pia kuwawezesha kuelimisha wananchi wenzao ni bora zaidi na ni jambo tunalohitaji kufanya hata zaidi. Ndio maana tunalenga sana maendeleo yanayohusisha uimarishaji wa ujuzi katika eneo la Geita. Tunahitaji kuimarisha vipengele vya usambazaji wa ndani ili kuunda duru muhimu ya biashara na kuinua uchumi.

Elimu ni mojawapo tu ya sekta ambazo tutazidi kuwekezea katika siku zijazo. miundo msingi, ni sekta nyingine. Mradi wa Maji wa Mji wa Geita (The Geita Town Water Project) unadhahirisha juhudi zetu za kuhakikisha kwamba wanajamii wa Geita wanapata maji safi na salama. Asilimia ya wanaopata maji mjini Geita imeongezeka kutoka asilimia 3 katika mwaka wa 2012 hadi asilimia 36 katika mwaka wa 2016, na kutokana na haya, huduma ya maji imeboresha afya ya watu na karibu magonjwa yote yanayohusiana na maji yametokomezwa. GGML itazidi kubuni hali zinazohitajika ili watu wengi zaidi waweze kupata maji katika miaka 5-10 ijayo. GGML ina miradi ya kijamii itakayogharimu dola milioni 53 ambayo imepangwa kwa miaka 14 ijayo.

Huku tukiendelea na shughuli hizi, tuna matumaini kwamba siku zijazo zitakuwa bora. Tunapoendelea kutekeleza kazi za uchunguzi katika GGM, tunatarajia kubadili uchimbaji kutoka ule wa shimo wazi hadi ule wa chini ya ardhi ili kuendeleza maisha ya mgodi na kufikia uwezo wake wote. GGML imewekeza dola milioni 713 nchini Tanzania katika miaka mitano iliyopita, na – pamoja na usaidizi wa wadau wetu wa ndani – tumeamua kuwekeza zaidi ili kuhakikisha maendeleo endelevu ya operesheni zetu. Isitoshe, kiwanda kipya cha kawi cha dola milioni 43 cha 3,948 MW, tulichowekezea, kinachotarajiwa kuwepo mtandaoni katika mwaka wa 2018, ni dhihirisho thabiti ya kujituma kwetu kwa muda mrefu nchini.

Maono yetu ya siku za usoni ni dhahiri. AngloGold Ashanti itazidi kuendeleza GGM ili iwe mali ya kiwango cha kiulimwengu nchini Tanzania, huku ikichangia pakubwa kwa Pato la Taifa na kuyapa kipaumbele maendeleo ya kijamii na kuunda nafasi za kazi. Kazi yetu ni kuendeleza kampuni ya uchimbaji inayoelekezwa na maadili, inayowasaidia watu na jamii zake ili kuleta ustawi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

Srinivasan Venkatakrishnan,
CEO